Maji nitayateka
Karaini nitayaweka
Kabla mwilini kuyaweka
Naanza kutetemeka
Baridi inaniteka
Viguzibampu vinazukaa
Mguu niponye natoka
Chumbani najipata
Kula ni lazima
Kunywa ni lazima
Kuoga si lazima
Na kama ni lazima
wanipe pesa ndoo nzima
Eti niende oga ndoo nzima
Akili yangu Ni nzima
Siezi oga maji ndoo nzima
Kuoga sasa Ni tabu
Mpaka upige mahesabu
Ukijiogea bila hesabu
Baridi itakuadhibu
Nifanyeje kina babu
Naomba niipewe jibu
Sijawasikiani mababu
Mii nataka wasia
Kwani kuoga mi nasusia
Sitaoga hata na wasia
Asante kwa kutonipa jibu
Sasa nafurahia
Sitaoga bila aibu
Kwani kuoga Ni tabu
Mpaka nipige mahesabu
No comments:
Post a Comment